Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Museveni atoa siri yake na Kawawa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

RAIS Yoweri Museveni wa Uganda ametoboa siri kwamba chama chake cha National Resistance Movement (NRM) kilipata baraka zote kutoka Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Julius Nyerere kilipokuwa kinaanzishwa.

Museven alisema hayo jana wakati akitoa salamu za rambirambi kwenye mazishi ya hayati Rashid Mfaume Kawawa, yaliyofanyika jana, Madale, jijini Dar es Salaam.

Alisema Serikali ya Tanzania iliifadhili NRM kifedha, msaada ambao ulisaidia kwa kiwango kikubwa kuanzishwa kwake.

Salamu hizo za rambirambi ambazo zilisomwa na mwakilishi wa Museveni, Elia Kategaya zilisema Serikali ya Tanzania ilikuwa ikitoa fedha hizo moja kwa moja kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuwapatia.

Hata hivyo, alisema kulikuwa na matatizo katika kuzifikisha salama fedha hizo kwa sababu mara kadhaa walikuwa wanaporwa njiani.

Alisema Kawawa kwa kushirikiana na Mwalimu Nyerere walitoa mchango wao mkubwa katika kuhakikisha chama hicho cha siasa kinaundwa.

Alisema lengo la kuunda chama hicho lilikuwa ni kuung'oa madarakani uongozi wa dikteta Iddi Amin Dada. Baada ya chama hicho kuundwa harakati za kuung'oa uongozi wa Iddi Amini ulianza ambapo mwaka 1979 Iddi Amin aliivamia Tanzania na kutangaza kwamba Kyaka Mkoa wa Kagera ni sehemu ya Uganda.

"Kutokana na kitendo hicho Jeshi la Tanzania lilimpiga Iddi Amin na majeshi yake na hatimaye Nyerere alimrudisha Milton Obote kuwa Rais wa Uganda kwa kupitia chama cha NRM kilichoundwa kwa msaada wa Serikali ya Tanzania," alisema.

Tags:

0 comments

Post a Comment