Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mbunge adai mafisadi watengeneza kadi feki

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Mbunge adai mafisadi watengeneza kadi feki

Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hebert Mtangi amesema kuwa mafisadi wanatafuta kila njia ya kutaka kumwangusha ili asipate nafasi ya kugombea kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kutengeneza kadi feki za Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuanza kuzigawa katika baadhi ya vijiji jimboni humo.

Watu hao wanaodaiwa kusambaza kadi hizo wanatuhumiwa kwamba wamekuwa wakitumia muda mwingi kumfanyia hujuma na mbinu chafu za kutaka kumwangusha kwa kuwashawishi baadhi ya wananchi kupokea kadi hizo na kuzihifadhi kwa madai wataruhusiwa kushiriki upigaji wa kura za maoni za kumsaka mgombea ubunge wa chama hicho baadaye mwaka huu.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara na wananchi wa Kitongoji cha Jambe na baadae kwa wakazi wa Kijiji cha Kicheba A kilichopo Wilayani hapa, mbunge huyo alikiri kuelezwa na baadhi ya wananchi kuwa wapo watu waliowapelekea kadi za chama hicho wakiwarubuni wazitunze ili waruhusiwe kuingia katika mkutano wa upigaji wa kura za maoni za kumpata mgombea ubunge wa CCM wakati wao si wanachama.

“Ndugu zangu wana Jambe mafisadi wamepamba moto, wamekuja Muheza na sasa hivi wametengeneza kadi feki za CCM wanawarubuni watu kwa kuwapa kadi za chama eti wakae nazo wataruhusiwa kuzitumia katika upigaji kura za maoni ili wafanikiwe kuniangusha…Lakini wakija wafikishieni ujumbe kwamba hawatafanikiwa ng’o! kwani ningejua wapi kama si wananchi wangu wananiambia wakiletewa hizo kadi,"alisema Mtangi.

Kutokana na hujuma hiyo mbunge huyo amewashauri wananchi na wanachama wa CCM kuwaumbua mafisadi hao kwa kuzipokea kadi hizo na kutoa taarifa za ujio wao sehemu husika ikiwamo viongozi wa chama na hata kuwapa taarifa watu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru).

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Tags:

0 comments

Post a Comment