Bunge la Afghanistan lakataa mawaziri walioteuliwa na Karzai
KABUL
Bunge la Afghanistan limewakataa zaidi ya theluthi mbili ya mawaziri walioteuliwa na Rais Hamid Karzai, wakiwemo washirika wake wawili wakubwa. Bunge hilo limewakataa mawaziri waliopendekezwa kuziongoza wizara za sheria, biashara, nishati, uchumi, afya ya jamii na mawasiliano.
Aidha, bunge hilo pia limemkataa mwanamke pekee aliyeteuliwa katika baraza la mawaziri, Husn Banu Ghazanfar, ambae hivi sasa ni waziri wa masuala ya wanawake. Ni mawaziri saba tu ndio walioidhinishwa na bunge hilo. Mawaziri wengi walioteuliwa na Rais Karzai walikuwa tayari katika baraza lake la mawaziri la awali na walikuwa wakiungwa mkono na mataifa ya Magharibi.
Ingawa Rais Karzai alishinda tena katika muhula wake wa pili katika uchaguzi ambao uligubikwa na udanganyifu, ameahidi kuunda serikali yenye ujuzi upesi iwezekanavyo na vile vile kukomesha rushwa nchini humo.
0 comments