Kisa cha Williamson
Hii leo kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni, Papa Benedikt wa 16 na mkuu wa shirika la usafiri wa reli la Ujerumani Deutsche Bahn, Hartmut Mehdorn, ndio waliomulikwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.
Tuanzie lakini Vatikan ambako uongozi umemtaka askofu anaefuata nadharia asilia Williamson arekebishe matamshi yake yanayokanusha mauwaji ya halaiki ya wayahudi-Holocaust, yaliyofanywa na utawala wa manazi. Siku moja kabla ya hapo alikua kansela Angela Merkel aliyemtaka kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni afanye hivyo. Ndo kusema kansela Angela Merkel amefanikiwa kupata kile alichokua akikitafuta kutoka kwa kiongozi mkuu wa kanisa katoliki la kirumi ulimwenguni? Linajiuliza gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linaloshuku kama kansela alikua na haki ya kufanya hivyo.
Kwa sababu hakumtaka Papa Benedikt wa 16 ajitenge na aina zote za hoja zinazokanusha au zinazowekea suala la kuuliza kuuliwa wayahudi wa Ulaya wakati wa utawala wa wanazi. Hayo Papa Benedikt wa 16 aliyatamka wiki moja kabla na mara kadhaa amekua akiweka wazi kabisa msimamo wake bila ya kuhitaji msaada kutoka Berlin.
Hata gazeti la Die Welt linahisi siasa ilikua nyuma ya lawama dhidi ya Papa. Gazeti linaendelea kuandika:
Bibi Merkel angeweza kupata njia ya kuwasilisha maoni yake kupitia balozi wa Ujerumani katika Vatikan Hans-Henning Horstmann. Njia ya kisiri siri, ambayo ingeachiwa serikali za nchi nyengine, ingekua na maana zaidi. Matamshi ya Williamson anaekanusha mauwaji ya halaiki ya wayahudi, Shoah, yamekosolewa moja kwa moja humu nchini. Upande huo lakini hakuna tofauti yoyote pamoja na kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni. Hali hiyo haijadhihirika hivyo lakini kutokana na matamshi ya kansela. Wakatoliki wanaweza kuingiwa na hasira na hali hiyo haitakua na matokeo ya kuvutia kwa bibi Merkel."
Mada ya pili magazetini hii leo ni kuhusu kisa cha kupelelezwa wafanyakazi wa shirika la usafiri la Deutsche Bahn. Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaandika:
Mehdorn anafanya kana kwamba data za wafanyakazi wake na ile hali ya kuvunjwa sheria zinazohusiana na kinga ya data,ni jambo dogo tuu linalokuzwa na kumpotezea wakati wa kuendelea na shughuli muhimu. Hatambui kama hii ni kadhia tete kabisa. Hatambui kwa sababu hathamini haki ya watumishi wake na wala hatilii maanani sheria. Anashindwa kutambua kwamba shirika la usafiri wa reli Die Bahn sio mamlaka ya mbali, bali shirika ambalo njia zake za reli zinakutikana katika ardhi ya nchi ya kidemokrasi inayoheshimu sheria-haki za kuhifadhiwa data na haki za wafanyakazi. Ikiwa Mehdorn angali ataamini anaweza kuvunja sheria atakavyo yeye, basi ajue pia kwamba anajitoa mwenyewe kazini."
0 comments