Inadaiwa wakoloni ndio walioeneza ukimwi. |
Wanasayansi wa Kimarekani walichunguza sampuli za awali kabisa za virusi vilivyowahi kugunduliwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mwaka 1959.
Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la Nature, umeonesha virusi hivyo huenda vilitoka kwa nyani na kumuingia binadamu kati ya mwaka 1884 na 1924.
Wanaamini wataalam hao kujengwa kwa miji mipya kulisababisha virusi hivyo kuzagaa.
Mgonjwa wa kwanza wa ukimwi aligunduliwa na madaktari mwaka 1981, lakini virusi vya HIV vimekuwepo kwa karne nyingi kabla ya wakati huo.
0 comments