Bw Manuel amekuwa akielezewa kuwa mhimili wa kuimarika kwa uchumi wa Afrika Kusini. |
Miongoni mwao ni waziri wa fedha, Trevor Manuel anayesifika kwa kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.
Wengine ni mawaziri wa ulinzi, usalama na ujasiriamali wa umma.Barua zao za kujiuzulu zimeidhinishwa na Bw Mbeki mwenyewe ambaye bado hajaondoka rasmi madarakani.
Kujiuzulu kwa makamu wa rais Bi Phumzile Mlambo-Ngcuka kulitangazwa mapema, naye akichukua hatua hiyo kumfuata rais Thabo Mbeki.
Kiongozi huyo aliyeng'olewa na chama chake hata hivyo amenukuliwa akisema atafungua kesi kupinga uamuzi wa mahakama kwamba aliingilia kesi dhidi ya Jacob Zuma.
Gavana wa Marekani ataka hatua za haraka kufufua uchumi
Gavana wa benki kuu ya Marekani, Ben Bernanke, ameonya kwamba masoko ya fedha duniani bado yanaendelea kuwa katika hali ngumu ya kibiashara.
Katika maelezo aliyoyandaa kwa kamati ya maswala ya fedha ya baraza la senate huko Washington, Bw Bernanke amelisihi baraza la Congress kuidhinisha haraka mpango wa kuokoa taasisi za kifedha zinazoyumba huko Marekani.
Amesema kuwa benki kuu ya Marekani, inaunga mkono kikamilifu mpango uliopendekezwa na utawala wa rais Bush kutoa dola bilioni 700 kuokoa mashirika hayo, zikiwa ni fedha nyingi zaidi katika historia kuwahi kutolewa kwa shughuli kama hiyo.
Lakini mwandishi wa maswala ya uchumi wa BBC anaeleza kuwa pamoja na mwitikio mzuri wa awali, idadi kubwa ya wajumbe wa Congress wameanza kuelezea mashaka kuhusu ufanisi wa mapendekezo hayo.
0 comments