Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Uwambukizaji HIV wapungua duniani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Kwa mujibu wa shirika la UNAids vifo vinavyotokana na maradhi ya Ukimwi vimepungua sana tangu kufikia kilele chake mwaka 2005 na kushuka kwa asili mia 21.
Ripoti ya mwaka huu ya UNAids inasema mwaka 2010 idadi ya maambukizo mapya ya HIV ilikuwa asili mia 21 ikiwa ni idadi iliyoshuka ikilinganishwa na ile ya mwaka 1997.
Shirika hilo limesema kuwa kushuka kwa uwambukizaji kumechangiwa na kupanuliwa na kurahishishwa njia za kupata huduma za matibabu.
Mkurugenzi wake Mkuu Michel Sidibe, amesema: "Kwa sasa tunaelekea kupata ufanisi mkubwa".
Aliongeza: "Hata wakati huu kuna msukosuko wa kiuchumi nchi mbalimbali zimeendelea kupata ufanisi katika kukabiliana na maradhi ya Ukimwi".
Utafiti huu wa sasa unasema kuwa idadi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi imefikia rekodi ya watu milioni 34.
Barani Afrika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara ndio mafanikio makubwa zaidi yameonekana ambapo asili mia 20 ya watu wamekuwa wakipata matibabu kati ya mwaka 2009 na 2010.
Nusu ya watu wanaofaa kupata matibabu hayo tayari wanashughulikiwa na kupata huduma hizi.
UNAids inakisia kuwa vifo vya watu 700,000 viliepukwa mwaka jana kutokana na kuwepo kwa huduma zifaazo za matibabu.
Huduma hizo pia zimesaidia sana katika kupunguza uwambukizaji kwa kuwa watu wanaozipata wanaoufahamu na inakuwa vigumu wao kuwaambukiza wengine.
Mwaka 2010 watu wanaokisiwa kufika milioni 2.7 waliambukizwa, idadi hii ikiwa imeshuka sana kutoka ile ya milioni 3.2 mwaka 1997 na watu milioni 1.8 walikufa kwa ukimwi ikiwa ni idadi iliyoshuka sana kutoka ile ya watu milioni 2.2 mwaka 2005.
Idadi hii inazidi kushuka kuambatana na ripoti za awali za UNAids.
Shirika hilo linasema: "Idadi ya watu waliopata maambukizi mapya ya HIV ni asili mia 30-50 ikiwa ni idadi ya chini zaidi ikiwa kama hakungekuwa na huduma za matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV."
Kuna baadhi ya nchi ambazo zimeonesha mafanikio ya hali ya juu.
Nchini Namibia, huduma za matibabu zimefikia asili mia 90 na utumiaji wa mipira ya Kondomu umeongezeka kwa asili mia 75, hii imesababisha kushuka kwa maambukizi mapya kwa asili mia 60 kufikia mwaka 2010.
UNAids inasema kuwa matokeo kamili ya ufanisi kuhusu matibabu haya huenda yakaonekana katika miaka mitano wakati nchi nyingi zaidi zitakuwa zimeimarisha huduma zake za matibabu.
Taarifa yake ilisema hata ikiwa maradhi haya hajakomeshwa kabisa: "kutokomezwa kwake kunaweza kuafikiwa ikiwa nchi zitawekeza ifaavyo kuhusu kukabiliana nao."

0 comments

Post a Comment