Akizungumza mjini Khartoum, Bwana Jalil alisema kuwa Sudan iliipelekea Libya silaha na risasi kwa kupitia Misri.
Serikali ya Sudan Kaskazini inapapambana na wapiganaji karibu na mpaka wake na Sudan Kusini, na katika jimbo la Darfur.
Waandishi wa habari wanasema kuanguka kwa utawala wa Kanali Gaddafi, kutaisaidia serikali ya Sudan kwa kuwanyima wapiganaji wa Darfur hifadhi.
Mustafa Abdel Jalil atafanya mazungumzo na wakuu kadha wa Sudan katika ziara yake ya siku mbili.

0 comments