Fabregas amefuzu uchunguzi wa afya yake aliofanyiwa mara mbili leo Jumatatu na atatambulishwa na klabu hiyo wakati wowote.
Uhamisho wa mchezaji huyo unakadiliwa kufikia paundi milioni 35, ambapo Arsenal itapokea kitita cha paundi milioni 30 na paundi milioni 5 nyingine zitatolewa kutegemea na idadi ya mechi atakazocheza na vikombe itakavyoshinda Barcelona.
Siku ya Jumapili, Arsenal na Barca walithibitisha makubaliano juu ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliyedumu klabuni hapo kwa takribani miaka nane.

0 comments