Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Nguvuni kwa kutishia kumuua Obama

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MSHIRIKA wa aliyekuwa kiongozi wa Mtandao wa Kigaidi Al Qaeda, Osama Bin Laden, Terry Kelly, amekamatwa nchini Ireland, kwa tuhuma za kutishia kumuua Rais Barack Obama wa Marekani

Kelly inayefahamika pia kwa majina ya Khalid Kelly na 'Taliban Terry' ni raia wa Ireland na inaamnika kuwa ni mfuasi wa muda mrefu wa Al Qaeda.Habari zinasema kukamatwa kwake, kunafuatia kutishia kumuua Rais Obama, wakati wa ziara yake nchini Ireland.

Kiongozi huyo wa Marekani, anatarajiwa kwenda Ireland wiki ijayo akiwa njiani kwenda kuhhudhuria mkutano wa viongozi wa mataifa makubwa kiuchumi duniani.Kwa mujibu wa polisi nchini humo, kabla ya kumkamata, Kelly alihojiwa kwa zaidi ya mara tatu kuhusu tishio lake dhidi ya Rais Obama.


Polisi walisema tishio Kelly kwa rai huyo, alilitoa kupitia katika mahojiano kati yake na gazeti la Mirror la Uingereza Jumapili iliyopita.Walisema katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti hilo, Kelly alisema yeye na kundi lake la Al Qaeda wana mpango wa kumuua Rais Obama wakati wa ziara yake na kwamba utekelezaji wa mpango huo unawezekana kwa sababu jeshi la nchi hiyo lina udhaifu.Alisema magaidi wanaweza kumlipa Dola za Marekani 1.4 milioni, mtu yeyote atakayekuwa tayari kumuua Obama.

Alisema tatizo ni kwamba yeye anafahamika mno na polisi wa Ireland, lakini vinginevyo ingekuwa ni rahisi kwake kumuua kiongozi huyo."Mimi mwenyewe ningejisikia vizuri kama Osama angemuua huyu adui mkubwa wa Uislamu lakini hata hivyo atakufa tu nitamuua,"alisema.Raia huyo wa Ireland, ni miongoni mwa waanzilishi wa Mtandao wa Al Qaeda akishirikiana na bin Laden.

Tayari Serikali ya Ireland tayari imeshaweka askari 10,000 kwa ajili ya kumlinda Obama na Malkia Elizabeth II, watapotembelea hiyo Jumanne, kwa ziara ya siku nne.

0 comments

Post a Comment