Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Kampala ulinzi mkali

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Serikali ya Uganda imeimarisha usalama katika mji mkuu Kampala,huku kiongozi wa upinzani  nchini Uganda Kizza Besigye, amekwama katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi, baada ya maafisa wa shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, kumzuia kupanda ndege.

Kiongozi huyo alikuwa akirejea nyumbani baada ya kupokea matibabu katika hospitali moja mjini Nairobi, kufuatia majeraha aliyoyapata wakati alipokamatwa na polisi wiki mbili zilizopita mjini Kampala.
Akiongea na BBC Dr. Besigye, amesema kuwa alifahamishwa na maafisa wa shirika hilo la ndege kuwa wameonywa wa serikali ya Uganda.'' wamenifahamisha kuwa serikali ya Uganda, imewaonya kuwa ndege hiyo haitaruhusiwa kutua ikiwa watamruhusu kama abiria. Sasa tunataka shirika la ndege la Kenya Airways ambayo ilikuwa na wajibu wa kuturudisha nyumbani, kuelezea rasmi sababu za kuzuiliwa kwao''
Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema, kurejea kwa Dr Besigye, siku moja kabla ya kuapishwa kwa rais Yoweri Museveni, kunatishia kuharibia sifa serikali ya nchi hiyo.
Serikali ya Uganda nayo inajiandaa kuwakaribisha viongozi wa nchi mbali mbali kwa sherehe ya kuapishwa ya rais Yoweri Museveni siku ya Alhamisi.
Rais Museveni ameonya wale wanaotaka kuvuruga shughuli hiyo yake kwamba watakabiliwa na sheria,rais alisema hayo akiwa nyumbani kwake magharibi mwa Uganda alipohutubia mkutano wa waandishi wa habari.

Yoweri Museveni
Museveni amesema kwa vyovyote vile hafla hiyo itaendelea, '' Nimeskia watu wengine,wanataka kusimamisha shughuli yangu,hakuna mtu atazuia hiyo shughuli labda Mungu peke yake,'' Alisema Museveni.
Aliongeza kusema kwamba kama viongozi lazima waheshimu serikali iliyochaguliwa kwa njia ya demokrasia ingawa alikiri kuwa polisi walipita mipaka wakati walipokuwa wanamkamata Kizza Besigye.

0 comments

Post a Comment