Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Washtakiwa wa Magufuli waangua kilio kortini

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
BAADHI ya washtakiwa katika kesi ya uvuvi haramu katika Bahari Kuu ya Tanzania, jana walimwaga machozi mahakamani wakililia dhamana.Hatua hiyo ilikuja  baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuwanyima dhamana.

Pamoja na kulia, washtakiwa pia walimkataa Jaji Razia Sheikh kwa madai kuwa hawana imani naye katika uendeshaji wa kesi hiyo na hivyo kumtaka ajitoe.Washtakiwa hao 36 ni raia wa mataifa ya China, Ufilipino, Vietnam na Kenya na wanakabiliwa na mashtaka ya kuvua samaki katika katika Ukanda wa Kichumi wa Tanzania  bila kibali.

Pia wanakabilia na mashtaka ya kuchafua mazingira ya bahari katika eneo hilo.Washtakiwa hao ambao kwa sasa wametimiza miaka  miaka miwili na siku 18 wakiwa rumande,  walifikishwa mahakamani jana ili kusikiliza uamuzi kuhusu maombi yao ya dhamana.

Awali walikuwa na  matumaini ya kuliona jua wakiwa nje kwa dhamana  lakini baadaye matumaini  hayo yaliyeyuka na kuwa huzuni iliyowalazimisha kumwaga machozi.

Kitendo hicho kilikuja baada ya Jaji Sheikh kuwanyima dhamana.Akitoa uamuzikuhusu maombi hayo,Jaji Sheikh alikubaliana na pande zote katika kesi hiyo kuwa dhamana ni haki ya msingi ya kila mshtakiwa kwa makosa yanayodhaminika.

Jaji Sheikh alisema kwa mazingira na asili ya kesi hiyo, hawezi kutoa dhamana kwa washtakiwa na kwamba uamuzi umezingatia angalizo la upande wa mashtaka wakati wa kusikilizwa kwa maombi hayo.

Jaji Sheikh alisema kuwa suala la kuwa na wadhamini wa kuaminika si sharti pekee la kuwapa dhamana washtakiwa hao na linahitaji pia vibali vya kuishi nchini.


Alisema hata hivyo, bado kuna maswali mahali wanapoweza kuishi ikiwa watu hao wataachiwa kwa dhamana na wakati wakisubiri kesi yao.

Huku akirejea uamuzi wa kesi mbalimbali zilizokwishakuamuriwa, na zenye mazingira sawa na kesi hiyo, Jaji  Sheikh alisema washtakiwa wote ni wageni wasiokuwa  na vibali vya kuishi nchini.

 
"Kwa mazingira,asili yake na unyeti wa kesi hii na adhabu inayoambatana na makosa yake, hakuna masharti ya kuridhisha kuwa wanastahili kupewa dhamana. Sijaridhika kuwa kama wakiachiwa hawataweza kutoroka," alisema.

Uamuzi huo ambaio baadaye ulitafsiriwa na wakalimani wa washtakiwa, ulisababisha watu hao o kutokwa na machozi huku wengine wakiina kwa huzuni.
Tags:

0 comments

Post a Comment