WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Said Amanzi kumfanyia uchunguzi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kudaiwa kupima eneo la ekari 7.5 huko Nyegezi na kuvimilikisha viwanja kwa viongozi maarufu, taasisi na rafiki zake bila ya kuwalipa fidia wenye eneo.
Kwa mujibu wa barua yenye kumbukumbu namba EA 71/17/6/01G ya Januari 26 mwaka huu ambayo iliandikwa na Kaimu Katibu wa Waziri, Brown Anyelwisye kwa maelekezo ya Waziri Tibaijuka, mkuu huyo wa wilaya ametakiwa kufuatilia suala hilo na kujua ni vipi Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza alifikia uamuzi wa kujimilikisha yeye kiwanja pamoja na kuwamilikisha watu wengine eneo hilo la familia ya Henry Nyamenda pasipo kuwaliwapa fidia ya ardhi yao.
“ Waziri amepokea barua kutoka kwa Henry Nyamenda anayelalamika kumilikishwa kwa viongozi wa serikali viwanja vyao akiwemo yeye mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza. Aidha mlalamikaji amebainisha kwamba eneo lake lingine la familia lenye ukubwa wa ekari 7.5 lilichukuliwa na Takukuru pasipo kulipwa fidia,” ilieleza barua hiyo.
Barua hiyo ambayo nakala yake tunayo imeeleza kuwa kuchukuwa maeneo ya watu na kupima viwanja na kisha kuwagawia wamiliki wengine bila ya kuanza kulipwa fidia ya ardhi ni kosa.
Ilieleza barua hiyo kuwa licha ya eneo kubwa la familia hiyo kugawiwa kwa Taasisi ya Kuzuia na kupamba na Rushwa (Takukuru) na Halmashauri hiyo kushindwa kuwalipa fidia familia hiyo, jambo hilo ni kosa na kinyume cha sheria Na. 5 ya fidia ya Ardhi ya mwaka 1999 kama inavyoelekeza.
Baada ya kupokea malalamiko ya familia hiyo Mheshimiwa Waziri ameniagiza nikuletee malalamiko haya ili uweze kuyachunguza na kuchukulia hatua stahiki, na tutafarijika kupata matokeo ya uchunguzi,” ilieleza barua huyo.
Familia hiyo imekiri kupata nakala ya barua hiyo kutoka kwa waziri, lakini Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe alikanusha kupokea kwa nakala ya barua hiyo na kusema kuwa hajui juu ya madai hayo na kwamba ndiyo kwanza anasikia kutoka kwa waandishi wa habari.
“Sina barua hiyo unayonileleza hivyo sijui lolote,” alieleza mkurugenzi huyo wa jiji alipoulizwa jana kwa njia ya simu.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana hakuweza kupatikana kutokana na kuwa nje ya ofisi, lakini mmoja wa maofisa wake anayeshughulikia utunzaji wa nyaraka za ofisi hiyo alikiri kufika kwa barua hiyo ofisi za mkuu wa wilaya na kukabidhiwa kwa mkuu huyo wa wilaya.
“Mie siyo msemaji lakini ni kweli barua hii imefika na mkuu anayo, atakuwa ameanza kuifanyia kazi kwa vile tayari amekwisha fanya vikao na baadhi ya wenyeviti wa mitaa wa mitaa ya Nyegezi juu ya malalamiko ya ardhi,” alieleza ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini kwa madai kuwa siyo msemaji wa ofisi.

0 comments