JUMUIYA ya Ulaya(EU) imetoa ripoti yake ya mwisho kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana na kuitaka Serikali iandae sheria itakayowapa haki wananchi kupinga matokeo ya urais mahakamani.
Kadhalika jumuiya hiyo imependekeza kuruhusiwa kwa wagombea binafsi, kwa maelezo kwamba kuwalazimisha wagombea kupitia kwenye vyama kunawanyima baadhi ya wananchi haki yao ya demokrasia ya kuchaguliwa.
Ripoti hiyo iliyosomwa na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi wa EU, David Martin, jijini Dar es Salaam jana, imetoa mapendekezo 30 yanayokosoa mwenendo mzima wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kwa ajili ya kuboresha mazingira ya uchaguzi ujao.
Tamko la EU limekuja wakati nchi ikiwa katika vuguvugu kubwa la mabadiliko, ambapo tayari Serikali imekubali kuanza kwa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.
Katiba inayotumika sasa imekuwa ikilalamikiwa kuwa haikidhi mazingira ya sasa na kwamba ni kikwazo cha utekelezaji wa demokrasia nchini.
Uchaguzi uliopita ulimpa ushindi wa asilimia 61 Rais Jakaya Kikwete wa CCM, huku ulipingwa vikali na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, aliyepata asilimia 27 akidai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ikishirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa ilivuruga matokeo hayo.
Kufuatia hali hiyo, wabunge wa chama hicho walitoka nje ya Ukumbi wa Bunge Rais Kikwete alipokwenda kuzindua Bunge la 10 mjini Dodoma mwezi Novemba mwaka jana, wakipinga taratibu zilizomwezesha kiongozi huyo kuingia madarakani.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 41 (7), mgombea urais akishatangazwa kuwa rais, hakuna mahakama yoyote inayoruhusiwa kuchunguza kuchaguliwa kwake na kipengele hicho ndicho kilisababisha Chadema kususia hotuba ya Rais kama hatua ya kukata rufaa kwa umma.
Mwaka jana Mtanzani, Denis Maringo, alifungua kesi mahakamani akitaka kipengele hicho kirekebishwe ili matokeo hayo yapingwe.
Taarifa ya EU iliyosomwa na Martin jana inaonyesha kuwa tayari wameshawasilisha mapendekezo hayo kwa viongozi wa Serikali ya Muungano na ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Mgombea binafsi
Kuhusu suala la wagombea binafsi, jumuiya hiyo imerejea wito wake wa kutaka haki ya wananchi kugombea kama wagombea binafsi iruhusiwe badala ya utaratibu uliopo sasa wa wagombea kulazimika kupitia kwenye vyama vya siasa.
Kesi kuhusu mgombea binafsi ilifunguliwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma mwaka 1993 na Mwenyekiti wa Democratic Party (DP) na Mchungaji Christpher Mtikila na ahakama hiyo kupitia kwa Jaji Kahwa Lugakingira ikaruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi.
Hata hivyo Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi hivyo alifungua kesi hiyo ya kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kushinda tena.
Lakini Serikali iliendelea kukata rufaa hadi mwaka 2010 Mahakama ya Rufani ilipotengua uamuzi wa Mahakama Kuu ambayo katika uamuzi wake ilisema mahakama haina uwezo wa kutengua kifungu cha katiba hivyo kuifanya Serikali kuibuka kidedea.
Mapendekezo ya mengine ya EU
Mapendekezo mengine ya EU ni pamoja na kupunguza kipindi cha kampeni kutoka miezi mitatu hadi mwezi mmoja, kwa maelezo kuwa kipindi hicho kinawachosha wapiga kura na kuvigharimu vyama vya siasa visivyo na uwezo kifedha.
Ripoti hiyo pia imesema kuwa NEC na ZEC zilikosa uwazi katika shughuli zao hasa katika hatua ya kujumlisha kura za wagombea.
“Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa EU umesikitishwa na kutokuwepo kwa uwazi kwa tume hizo upande wa Bara na Visiwani,” alisema Martin.
Alisema kuwa tume hizo zilipaswa kuchapisha na kusambaza nyaraka na vifaa vyote vya uchaguzi kwa wakati mwafaka, orodha za vituo vya kupigia kura, orodha ya majimbo na taarifa za matumizi ya fedha wakati wa kampeni.
Kuhusu tume hizo za uchaguzi, ripoti hiyo imependekeza kuwa, zisitawaliwe na maafisa wa Serikali hasa katika ngazi za mikoa ambapo hutumika watumishi wa Serikali wakti kitaifa makamishna wa tume wakiteuliwa na rais.
Badala yake Martin ameshauri ushirikishwaji wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi na asasi za kiraia katika tume hiyo.
Jumuiya hiyo imerudia wito wake wa kutaka haki ya wananchi kugombea kama wagombea binafsi iruhusiwe badala ya utaratibu wa sasa wa wagombea kulazimika kupitia kwenye vyama.
Pia imependekeza kuwepo kwa uwazi zaidi kwa vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na kuruhusiwa kufika kwenye maeneo ya uchaguzi siku ya kupiga kura.

0 comments