Habari zilisema hadi kufikia jana, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro, Chuo Kikuu cha Tumaini na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam, walikuwa bado hawajapata mikopo.
Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na gazeti hili walisema kitendo hicho kimewaathiri kisaikolojia na hata kulazimika kukopa fedha kutoka kwa watu.
Mwanafunziwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwesigwa Christian alisema kuchelewa kwa mikopo hiyo kumemfanya ashindwe kuhudhuria masomo.
"Mpaka sasa hatujapata pesa zetu, jambo linalotufanya tushindwe kuingia darasani kwa kukosa nauli na njaa," alisema Mwesigwa.
Alisema kwa jumla wanafunzi, wamechoshwa na utaratibu wa bodi hiyo katika kutoa mikopo na kuiomba serikali kuingilia kati jambo hilo.
"Kila tukija tunapangiwa tarehe na kupewa sababu zisizokuwa na msingi mara hatujajaza fomu, mara majina hayaonekani hatuelewi kwa kweli,"alisema Jonh Revocatus.
![](http://www.blogger.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
0 comments