IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
WAKATI Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ikisubiriwa kutangaza matokeo ya nafasi mbalimbali za uongozi ya uchaguzi mkuu uliofanyika jana nchini kote, baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wamekesha wakisimamia zoezi la kuhesabu kura.
Mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura wakazi hao walikaa karibu na vituo walivyopigia kura huku wakigoma kuondoka licha ya kutakiwa kufanya hivyo na vikosi vya ulinzi na usalama.
Mwananchi lilishuhudia makundi ya wananchi hao katika maeneo ya Sinza, Kawe na Ubungo, ambapo katika eneo la Mwananyamala Kisiwani, Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) walilazimika kukesha wakiwa katika magari matatu aina ya Land Rover (Difender) pamoja na gari la kumwaga maji ya kuwasha (Deraya).
“Sisi hapa hatuondoki maana tukifanya hivyo tu kura za mgombea wetu tuliyemchagua zitachakachuliwa, hawa wamezoea kila uchaguzi wanaiba kura, haiwezekani kabisa hatuondoki,” alisikika akisema mmoja wa wananchi hao.
You Are Here: Home - - Wakesha wakilinda kura zao
0 comments