Baada ya tambo za zaidi ya miezi miwili wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010, sasa ubishi umefika tamati baada ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete kuibuka kidedea.
JK amewashinda wapinzani wake wa karibu, Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA na Profesa Ibrahim Haruna Lipumba wa CUF.
Awali, ilidhaniwa kwamba Slaa angeweza kuandika historia mpya kwa kumuangusha JK, hivyo yeye na chama chake kuongoza serikali lakini matokeo yamekuwa kinyume chake.
Profesa Ibrahim Haruna Lipumba wa CUF.
Ushindi wa JK, unakuwa na maana kuwa taasisi za utafiti za REDET na SYNOVATE, zilikuwa sahihi kwenye matokeo yake kama zilivyowasilisha siku chache kabla ya uchaguzi.Hata hivyo, juzi, Slaa kupitia mwanasheria wa chama chake, Mabere Nyaucho Marando, aliandika malalamiko yake Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa matokeo yalichakachuliwa.
Slaa, alidai kuwa alihujumiwa katika hesabu ya majimbo mengi ndiyo maana matokeo yalicheleweshwa kutangazwa kila sehemu aliyoshinda.
Alisema, anayo hesabu kamili ya kura alizopata, kwahiyo kilichotangazwa na NEC ni udanganyifu.
Katika hatua nyingine, licha ya kuthibitika kwamba kimemomonyoka kwa kiasi fulani kufuatia idadi kubwa ya wabunge ambayo vyama vya upinzani vimepata mwaka huu, lakini bado CCM imeonesha jeuri kwa kuzoa majimbo yote yaliyochelewa.
Majimbo yote yaliyotangazwa juzi (Jumatano), hasa baada ya mvutano mkubwa kati ya wananchi na wakurugenzi wa uchaguzi na kulazimika dola kuingilia kati, yamekwenda CCM.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, kama yalivyotangazwa na wakurugenzi wa uchaguzi kutoka kwenye majimbo mbalimbali yapo kama ifuatavyo;
MOROGORO MJINI: Abdulziz Aboud (CCM).
Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA.
KONDOA KUSINI: Juma Nkamia (CCM).NEWALA: George Mkuchika (CCM).
KILOMBERO: Abdul Rajab (CCM).
MBINGA MASHARIKI: Casian Gaudence Kayemba (CCM)
TUNDURU: Mtara Ramo Makau (CCM).
MULEBA KASKAZINI: Charles Mwijage (CCM).
SINGIDA KASKAZINI: Lazaro Nyarandu (CCM).
TUNDURU KUSINI: Mtutura Abdallah Mtutura (CCM).
TUNDURU: Ramo Makau (CCM).
SEGEREA: Milton Makongoro Mahanga (CCM).
MKURANGA: Adam Kigoma Malima (CCM).
Awali, majimbo yafuatayo yalitolewa matokeo na kutangazwa kama ifuatavyo;
Jimbo la Bagamoyo
Shukuru Kawambwa (CCM)
Korogwe Mjini
Yusuph Nasir (CCM).
Kilwa Kaskazini,
Mustapha Mangungu (CCM).
Busanda
Laurensia Bukwimba (CCM).
Kilwa Kusini
Bungaro Said (CUF).
Igunga
Rostam Aziz (CCM).
Liwale
Faith Mohammed Mitambo (CCM).
Njombe Kaskazini
Deo Sangu ‘Jaha People’ (CCM).
Njombe Magharibi
Jerson Rweige (CCM).
Same Mashariki
Anne Kilango (CCM).
Same Magharibi
David Mathayo (CCM).
Mbulu
Mustapha Akonei (CHADEMA).
Urambo Magharibi
Juma Athman Kapuya (CCM).
Lindi Mjini
Salum Balhan (CCM).
Namtumbo
Vita Kawawa (CCM).
Kwimba
Sharif Mansoor (CCM).
Siha
Aggrey Mwanri (CCM).
Ileje
Nikusama Kibona (CCM).
Korogwe Vijijini
Steven Ngonyani (CCM).
Yanaendelea uk. 14
Inatoka uk. 2
Muhambwe
Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi).
Longido
Michael Lekule Laizer (CCM).
Jakaya Kikwete CCM.
Kwa jumla, wapinzani walioshinda Tanzania Bara ni hawa;1.Halima James Mdee -Kawe/Chadema
2.Tundu Lissu - Singida Mashariki/Chadema
3. Mustapha Quorro Akonaay- Mbulu/Chadema
4. Israel Yohana -Karatu/Chadema
5. John Mnyika -Ubungo/Chadema
6.Silinde David -Mbozi Magharibi/Chadema
7. Felix Mkosamali -Muhambwe/NCCR Mageuzi
8.Salvatory Naluyaga Machemuli-Ukerewe/Chadema
9.Agripina Z. Buyogela -Kasulu Vijijini/NCCR-Mageuzi
10.Ole Sambu -Arumeru Magharibi/Chadema
11.Augustine Lyatonga Mrema-Vunjo/TLP
12.Salum Barwani -Lindi/CUF
13.Joseph Mbilinyi -Mbeya Mjini/Chadema
14.Philemon Ndesamburo Kiwelu-Moshi Mjini/Chadema
15.Dk Antony Mbasa -Biharamulo Magharibi/Chadema
16.Machali Moses John-Kasulu Mjini/NCCR Mageuzi
17.Joseph Selasini -Rombo/Chadema
18.Hezekiah Wenje -Nyamagana/Chadema
19.Peter Msigwa -Iringa Mjini/Chadema
20.Freeman Mbowe -Hai/Chadema
21.Vincent Nyerere -Musoma Mjini/Chadema
22.Godbless Lema -Arusha Mjini/Chadema
23.Zitto Kabwe/C -Kigoma Kaskazini/Chadema
24.Hayness Samson -Ilemela/Chadema
25.John Shibuda -Maswa Magharibi/Chadema
26.Meshack Opulukwa -Meatu/Chadema
27.Sylvester Kasulimbayi Mhoja-Maswa Mashariki/Chadema
28. John Cheyo -Bariadi Mashariki/UDP
29. Bungaro Said -Kilwa Kusini/CUF
30. David Kafulila -NCCR Mageuzi
0 comments