Mkutano huo uliofanyika katika ofisi ya waziri mkuu umefuatia taarifa ya kanali Charles Andrianasoavina kwamba tume ya kijeshi inayolinda maslahi ya raia nchini humo imeundwa kuchukua mamlaka ya taifa hilo ambalo wanachi wake wanaendelea kupiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya hii leo.
Kiongozi wa taifa hilo aliyeingia pia madarakani kupitia mapinduzi, akisaidiwa na jeshi mwaka jana, Andry Rajoelina, hajulikani aliko, ingawa inasadikiwa kwamba yuko Antananarivo, mji mkuu wa Mdagascar.
Inasemakana kwamba wananchi wengi wanaopiga kura ya maoni kuhusu katiba hawana taarifa juu ya kupinduliwa serikali.Wapinzani wa Rajoelina wanaipinga katiba hiyo ambayo wanadai itampa madaraka zaidi ya kuendelea kubabakia uongozini.

0 comments