Shirikisho la soka duniani FIFA
limeisimamisha kwa muda Nigeria kushiriki katika mashindano ya kimataifa kutokana na serikali kuingilia kati mchezo huo.Shirikisho la soka duniani FIFA
Uamuzi huo ulifanyika Jumatatu baada ya wajumbe kadhaa wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF) kufikishwa mahakamani.
Sheria za FIFA zinakataza serikali kuingilia kati wanachama wake.
"kamati ya dharura ya FIFA imeamua leo....kusimamisha NFF mara moja kutokana na serikali kuingilia kati," FIFA ilisema.
"wakati wa kusimamishwa kwa muda,shirikisho la NFF halitawakilishwa kwenye mashindano ya kanda,bara Afrika au kimataifa, pamoja na mechi za kirafiki," taarifa hiyo ya FIFA ilisema.
Kufwatia marufuku hii ya Nigeria ya kutocheza mechi za kimataifa,sasa hatma ya mechi ya wikiendi hii dhidi ya Guinea mjini Conakry haijulikani.
0 comments