Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - FEMACT WAIJIA JUU SERIKALI

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mwanaharakati kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Francis Kiwanga akisoma tamko hilo la FemAct.
Muungano wa mashirika 50 yanayotetea Usawa wa Kijinsia, Haki za Binadamu, Maendeleo na Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi (FemAct) leo umekutana na kutoa tamko la kulaani tishio la serikali la kutishia kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mwanahalisi kwa madai kuwa yanaandika habari za uchochezi dhidi ya serikali iliyoko madarakani. 

Katika tamko hilo lililotolewa katika Makao Makuu ya Mtandao wa Jinsia nchini (TGNP), Mabibo Dar es Salaam, FemAct pia wamelaani vikali vitisho vilivyotolewa na katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kwa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA wa kuwataka wasijishughulishe na masuala ya siasa hasa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 30 mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Ananilea Nkya akimdokeza jambo Francis Kiwanga wakati wa mkutano wa FemAct na waandishi wa habari, leo.
Wadau wakibadilishana na mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Ananilea Nkya.
Mahali ulipofanyika mkutano uliopitisha azimio hilo, Mabibo jijini Dar es Salaam.



PICHA: HASHIM AZIZ/GPL
Tags:

0 comments

Post a Comment