Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wakenya watumikia kufundisha Watanzania Katiba ya Tanzania. Hali ya Hewa yachafuka

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MWENYEKITI wa Chama cha TADEA, John Chipaka, jana alichafua hali ya hewa kwenye kongamano la kujadili ushiriki wa walemavu kwenye uchaguzi mkuu ujao, baada ya wakufunzi kutoka Kenya kutumika kufundisha Watanzania mada mbalimbali ikiwamo ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kongamano hilo lililofanyika kwa siku tatu mfululizo na kumalizika jana Dar es Salaam, lilishirikisha viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa vya nchini kwa usimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Taasisi ya Kimataifa inayojishughulisha na masuala ya uchaguzi (ERIS).

Kwa vile mada nyingi zilihusu ushiriki wa wananchi wakiwamo watu wenye ulemavu katika uchaguzi mkuu, wakufunzi waliotoa mada ambao wengi walikuwa Wakenya, walilazimika kutumia vifungu ndani ya Katiba ya Tanzania, vinavyozungumzia masuala ya uchaguzi ili kuelimisha washiriki haki za Watanzania katika uchaguzi.

Wakati mada zikiwa juu ya uchaguzi mkuu ujao nchini, Msimamizi Mkuu wa Kongamano hilo, alikuwa Njeri Kabeberi wa Kenya, Msimamizi Msaidizi, Sara Muhoya wa Kenya wakati wakufunzi walikuwa Louis Otieno na Salome Muigai wote kutoka Kenya.

Kutoka Tanzania walikuwa ni Mtangazaji wa BBC Zanzibar, Ally Saleh na Mbunge wa Kuteuliwa na Rais aliyemaliza muda wake Al Shaymaa Kwegyir.

Mara baada ya kukamilika kwa kipindi cha utoaji mada, Muhoya aliwapa fursa washiriki kuchangia hoja au kuuliza maswali, kutokana na mada zilizowasilishwa na wakufunzi, na baada ya kupewa nafasi, Chipaka hakusita kutoa dukuduku lake la kutopendezwa

kwa hatua ya Wakenya kutumika kuwa wakufunzi katika kongamano hilo.

“Mara ya kwanza hawa ERIS walituletea walimu Wazungu kutufundisha kuhusu uchaguzi wetu na Katiba yetu.

Leo tena naona wamejaa walimu Wakenya wanatufundisha kuhusu uchaguzi wetu na Katiba yetu, badala ya Watanzania waliobobea kwenye siasa,” alihoji Chipaka.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alifika mbali zaidi kwa kusema Wakenya hawapaswi kuwaeleza Watanzania suala lolote kuhusu demokrasia na muundo wa Katiba kwa vile Kenya na Zimbabwe ni mataifa yaliyokufa kidemokrasia na ndiyo maana yamekuwa yakitawaliwa na vurugu wakati wa uchaguzi.

Mchango huo wa Chipaka kwa kiasi kikubwa ulianzisha malumbano ambapo wakufunzi hao wa Kenya walijibu hoja hiyo kwa vijembe hatua iliyomfanya pia Meneja wa Kongamano hilo, Njeri, kusimama na kumtuhumu Chipaka kwamba mara nyingi amekuwa akianzisha ubaguzi wa Watanzania na Wakenya kila anapoandaa semina.

“Wewe mzee (Chipaka) mara zote nikiandaa semina umekuwa unakuja, lakini kila mara umekuwa unatusakama sisi Wakenya.

Kama tungekuwa tunafundisha vibaya ni kwa nini unakuja? Kenya na Tanzania ni mataifa jirani na mara zote tumekuwa tunafurahi katika semina zetu, lakini mwishoni wewe unatutoa machozi, sasa leo hatulii kwa ajili yako,” alisema Njeri.

Malumbano hayo yalimfanya Mratibu wa Uwezeshaji Vyama vya Siasa wa UNDP, Msemo Mavale, kusimama na kutoa ufafanuzi wa suala hilo ambapo alianza kwa kummwagia sifa Chipaka, kuwa ni kiongozi wa kitaifa wa chama cha siasa, ambaye mara zote amekuwa akishiriki kwenye mikutano inayoandaliwa na UNDP.

“Huyu mzee nampongeza sana, ni mtu ambaye hawezi kukaa na dukuduku hata siku moja, yeye anataka jambo likimwuma alitoe hapo hapo.

Ni kiongozi wa siasa pekee ambaye amewahi kumpinga hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hadharani bila woga.

Kama aliweza kufanya hivyo wakati wa chama kimoja unadhani sasa atahofu nini?”

Mavale akazungumzia hatua ya kongamano hilo kuwa na wakufunzi wengi kutoka Kenya kuwa ni matokeo ya manufaa ya Soko la Pamoja la Nchi za Afrika Mashariki, ambapo baada ya kazi hiyo kutangazwa kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje, wakufunzi hao kutoka Kenya ndio walioshinda zabuni hiyo.

“Hii ni changamoto kwetu na sisi Watanzania kuangalia namna tunavyoweza kulitumia Soko la Pamoja kupata kazi mahala pengine ikiwemo Kenya na si kukaa na kulalamika tu,” alisema.

Alisema UNDP imewahi kuandaa makongamano kama hayo siku za nyuma na mara nyingi idadi kubwa ya walimu ilikuwa ni Watanzania, hadi juzi baada ya zabuni hiyo kutangazwa na Wakufunzi kutoka Kenya kushinda
Tags:

0 comments

Post a Comment