Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Rais wa Iran asema Marekani ndio iliyojishambulia yenyewe Sept. 11

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter NEW YORK:


Ahmedinejad wa Iran alihotubia baraza hilo na dakika chache baadae wajumbe wa Marekani walitoka kwenye ukumbi huo, wakifuatwa na wajumbe wengine wa nchi za Ulaya ya Magharibi.


Ahmedinejad alizungumzia juu ya nadharia kuwa serikali ya Marekani ndio iliyohusika na shambulio la Septemba 11 ili iweze kujiimarisha zaidi katika Mashariki ya Kati pamoja na kuimarisha uchumi wake.



Obama atoa mwito kusaidia mchakato wa amani Mashariki ya Kati


Rais wa Marekani Barack Obama ametoa mwito kwa viongozi wa kimataifa kusaidia jitahada za kutafuta suluhisho la amani kumaliza mgogoro kati ya Waisraeli na Wapalestina. Alipohotubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Obama alisema, ni muhimu kwa pande zote kushirikiana ili katika kipindi cha mwaka mmoja ujao,kuweze kupatikana taifa huru la Palestina na Israel inayoweza kuishi kwa usalama.
O-TON: OBAMA:
Rais Obama akisema "amani yapaswa kupatikana kati ya Waisrael na Wapalestina, lakini kila mmoja wetu pia anawajibika kutoa mchango wake."
Tags:

0 comments

Post a Comment