Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - MREMA ACHONGEWA KWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS MOROGORO

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

MREMA ACHONGEWA KWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS MOROGORO



Mzee Juma Kitunga akimchongea Mrema kwa mgombea mwenza wa urais TLP.
NA DUNSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
WAFUASI wa Chama cha Tanzania Labour Party [TLP] Mkoani hapa wamemchongea mgombea ubunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kupitia chama hicho, Bw. Augustino Lyatonga Mrema kwa mgombea mwenza wa Urais wa Chama hicho Bw. Abdallah Othman Mgaza.

Mgombea mwenza huyo wa urais kutoka Unguja alipokea malalamiko hayo kwenye mkutano wa kampeni wa chama hicho uliofanyika jana eneo la Masika na kwamba mara baada ya mgombea mwenza huyo kumaliza kuwahutubia wananchi wachache waliojitokeza kwenye mkutano huo, aliruhusu kuulizwa maswali yasiozidi matatu.

"Nimemaliza kuzungumza naomba kama miongoni mwenu kuna mtu yoyote mwenye swali aniulize," alisema mgombea mwenza huyo ambaye mara baada ya kutoa kauli hiyo mzee Rajabu Athumani alikuwa wa kwanza kumuuliza swali mgombea huyo ambapo aliuliza: "Nimesikia sera na ahadi nyingi za wagombea, lakini nimesikitika hawagusii suala la mkulima wa jembe la mkono anayeishi vijijini kwamba watamsaidia vipi, wewe hapa umesema mambo mengi mazuri lakini pia hilo hukuligusia, ni kwanini?" aliuliza mzee Athumani.

Swali la pili ambalo liliulizwa na Mzee Juma Kitunga lilikuwa hivi: "Mheshimiwa mimi ni mfuasi mzuri sana wa TLP lakini mimi na wenzangu tumechanganywa sana na kauli ya Mrema ambaye anagombea ubunge kule Vunjo Moshi kupitia chama chetu, ambapo amewataka wananchi wa Vunjo kumpa kura za ubunge yeye na za urais amewaagiza wampe swahiba wake Jakaya Kikwete, wakati chama chetu kina mgombea urais"

Akijibu swali hilo lililoonekana kumchanganya mgombea mwenza huyo alisema "Ni kweli nilitegemea kusikia swali hilo kwenye mikutano yangu ya kampeni lakini niwatoe wasiwasi kwamba Mrema ni kweli alisema hayo lakini tumuache kama alivyo na swahiba wake huyo Kikwete" alisema Mgaza kwa ufupi.
Mzee Rajab Athumani akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Mgombea ubunge wa mwisho kulia akiwa na wagombea udiwani sita wa chama hicho.
Bango lenye picha ya mgombea urais pamoja na mgombea mwenza kwa tiketi ya chama hicho.
Tags:

0 comments

Post a Comment