Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mkemia Mkuu afariki dunia

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dk. Ernest Mashimba, ameaga dunia jana akiwa hotelini wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Dk Mashimba alikwenda Lushoto kuhudhuria mahafali ya mwanawe aliyemaliza kidato cha nne katika Sekondari ya Kifungilo.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Sophia Mjema, amethibitisha kwamba, Dk Mashimba ameaga dunia.

Kwa mujibu wa Mjema, kiongozi huyo alikufa bafuni katika Hoteli ya Lushoto Executive Inn.

Mjema amesema, Dk. Mashimba alifika Lushoto Ijumaa, na kesho yake (Jumamosi) alikwenda katika mahafali hayo.

Amesema, wafanyakazi wa hoteli hiyo walipotaka kufanya usafi chumbani kwake, walishindwa kuingia, wakatumia funguo za ziada kuingia na kumkuta bafuni akiwa amekufa.

Mjema amesema, mwili wa marehemu Mashimba uliletwa Dar es Salaam jana kwa ajili ya uchunguzi.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Liberatus Sabas, alisema, baada ya kuutoa mwili wa Dk. Mashimba katika hospitali hiyo, ulipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto.
Tags:

0 comments

Post a Comment