Israel yashambulia vituo katika Ukanda wa Gaza
Mtu mmoja aliuawa na wengine watatu walijeruhiwa katika mashambulio mawili dhidi ya njia inayopitia chini kwa chini kuelekea Misri ambayo hutumiwa kwa biashara haramu.
Shambulio la tatu lililenga ngome ya zamani ya kundi la Hamas katika mji wa Khan Yunis ulio kusini mwa Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel limethibitisha kufanya mashambulio hayo.Imechukua hatua hiyo kujibu mashambulio mapya ya makombora yaliyolenga makaazi ya Wayahudi hivi karibuni kutoka kusini mwa Ukanda wa Gaza.

0 comments