NEW YORK
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi Antonio Guterres amesema mzozo unaondelea nchini Kyrgyztan huenda ukasababisha janga kubwa la kibinaadamu iwapo jumuiya ya kimataifa haitoingilia kati.
Ametaka jumuiya ya kimataifa kutoa msaada wa kijeshi, akisema kuwa serikali ya Kyrgystan imeshindwa kudhibiti ghasia na mapigano yanayoendelea.
Wakati huo huo Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa limeanza kusambaza misaada ya chakula kwa wakaazi wa mji wa Osh.
Mapigano makali kati ya makabila mawili ya WaKyrgyzi waliyo wengi na waUzbeki waliyo wachache yamesababisha takriban watu robo millioni kuyahama makazi yao.Kiasi ya watu elfu 75 walikimbilia katika nchi jirani ya Uzbekistan, kabla ya mpaka wa nchi hiyo kufungwa.
0 comments