Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA MICHEZO - Yanga wagawa kadi familia ya Karume

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, jana ulimkabidhi mke wa rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Fatma Karume, kadi namba 2 ya uanachama, hafla iliyofanyika makao makuu, Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kadi hiyo ni kwa ajili ya kutambua mchango wa mume wake, hayati Abeid Amani Karume katika maendeleo ya michezo hapa nchini.
Mbali ya Fatma, pia Yanga walikabidhi kadi namba 3 kwa mke wa rais wa sasa wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, Shadya Karume.
Hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na msafara wa Wanayanga 80 kutoka Zanzibar, ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha Rais Abeid Karume kitakachokumbukwa Jumatano, Aprili 7.
Pia wanachama wa Yanga walimuomba Mama Fatma awe mdhamini wa klabu hiyo, ombi ambalo alilikubali.

0 comments

Post a Comment