IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
WAKATI fulani Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema yuko tayari kusulubiwa kuliko kuzungumzia masuala ya kampuni za Tangold, Meremeta na Mwananchi, lakini msimamo huo haukumzia mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa kuibua tena swali kuhusu kampuni hizo, akitaka hatima ya malalamiko ya wabunge.
Mara kadhaa, Dk Slaa amekuwa akimbana Pinda kuhusu kampuni hizo zinazolalamikiwa kuwa zilichota mabilioni ya fedha za walipa kodi kwa njia za kifisadi, lakini serikali imekuwa ikieleza kuwa kampuni hizo zinahusu masuala ya usalamwa taifa na hivyo hayawezi kuzungumziwa hadharani.
Na alipobanwa sana, Pinda alijibu yuko tayari kusulubiwa.
Jana Dk Slaa aliibua tena hoja hiyo katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu na kumtaka kiongozi huyo wa shughuli za serikali bungeni aeleze hatima ya sakata la kampuni hizo.
Dk Slaa, ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema, alisema kuwa kwa karibu mwaka mmoja sasa tangu ufisadi huo ulipoibuliwa, kumekuwa na kauli mbalimbali kuhusu kampuni hizo ambazo haziridhishi na ambazo wakati fulani mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliwahi kuziita za ovyo.
Kutokana na hali hiyo, Dk Slaa alimtaka waziri mkuu atoe tamko la serikali pamoja na kufafanua hatua ilizofikia katika kuwashughulikia wahusika wa ufisadi huo.
Swali hilo lilimfanya waziri mkuu, maarufu kama mtoto wa mkulima, kupatwa na kigugumizi kujibu akieleza kuwa hawezi kuwa na majibu ya moja kwa moja kuhusu kampuni hizo.
“Ndugu yangu Dk Slaa anajua siwezi kuwa na majibu ya moja kwa moja, ila ninachoweza tu kusema ni kuwa maeneo ambayo serikali imeshayafanyia kazi na jitihada zake zimeanza kuonekana," alisema Pinda.
"Pia yapo yale ambayo bado yanaendelea kufanyiwa kazi.â€
Hata hivyo pamoja na majibu hayo, Dk Slaa aliuliza swali la nyongeza akitaka Pinda atoe tamko kuhusu ufisadi huo kwa kuwa ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.
“Waziri mkuu ninakuheshimu sana, kwa vile katiba inasema wewe ndiye msimamizi wa serikali hapa bungeni, usipojibu wewe maswali haya magumu nani atajibu," aliuliza Dk Slaa.
"Basi ninakuomba utoe tamko kuhusu jambo hili bungeni na maeneo yaliyoshughulikiwa.â€
Lakini, hata hivyo waziri mkuu hakuweza kufafanua zaidi kuhusiana na eneo ambalo limeshughulikiwa na serikali na lile ambalo bado huku akisisitiza kuwa kauli alishatoa na kwamba serikali imeshachukua hatua.
Pinda alisema hatua hizo ni pamoja na za kimahakama katika masuala yaliyohusu sheria na kumuomba Dk Slaa aeleze iwapo kuna mahali ambapo anadhani bado serikali haijashughulikia.
“Ndugu yangu, kama unataka kauli nimeshaitoa. Nimeeleza kuwa yapo mambo ambayo tayari yameshughulikiwa na kufikishwa mahakamani, kama bado kuna mengine, itoshe kusema kuwa serikali itaendelea kuyafanyia kazi na kuyashughulikia,†alieleza Waziri Pinda.
Dk Slaa amekuwa akiibua sakata la makampuni hayo kila mara na mwaka jana alikumbwa na vikwazo kadhaa wakati alipotaka kusoma maoni ya kambi ya upinzani kuhusu hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wakati huo, Spika Samuel Sitta alitangulia kumuonya kuhusu mambo kadhaa, ikiwemo matumizi ya maneno dhidi ya rais wa zamani na suala hilo la kampuni hizo, hali iliyomfanya mbunge huyo wa Karatu kuruka sehemu nyingi za hotuba yake.
Hata hivyo, alihoji suala la kampuni hizo tatu na Spika Sitta alilimaliza kwa kumwambia kuwa walishakubaliana kwenye vikao vya kamati za Bunge kuwa masuala yanayohusu jeshi yasizungumziwe hadharani.
You Are Here: Home - - Slaa amkumbusha Pinda machungu ya Deepgreen
0 comments