Ikiwa maswala nyeti kwenye katiba hiyo, yakiwemo sheria kuhusu utoaji mimba, mahakama za kadhi na sheria za kumiliki ardhi, hayatapatiwa ufumbuzi, baadhi ya wabunge nchini Kenya wanapania kuwashawishi Wakenya kupiga kura kuikataa katiba mpya iliyopendekzwa, huku kura ya maoni kuhusu katiba hiyo ikitarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.
Siku ya Alhamisi Aprili 8 mwaka huu, rais wa Kenya Mwai Kibaki, waziri mkuu Raila Odinga na makamu wa rais, Kalonzo Musyoka, walikutana na viongozi wa dini ya Kikristo kujaribu kusuluhisha mzozo uliojitokeza kuhusu kipengee kinachozungumzia utoaji mimba na mahakama za kadhi.
Viongozi wa makanisa wameapa kufanya kampeni ya kupinga vipengee hivyo ndani ya katiba hiyo havitafanyiwa marekebisho.
Josephat Charo amezungumza na Bi Jebii Kilimo, mbunge wa jimbo la Marakwet Mashariki, ambaye anaipinga katiba hiyo, na kwanza kumuuliza tatizo liko wapi.
0 comments