Imeelezwa kuwa mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa tumbo ndipo Dk. Andrew alimwandikia kipimo cha Utra Sound.
Kwa mujibu wa mgonjwa huyo, alifika hospitalini hapo majira ya jioni na baada ya kueleza tatizo lake, Dk Andrew alimwandikia kipimo hicho,baada ya kuingia katika chumba cha kufanyiwa kipimo, ndipo daktari huyo alimpa kitu kilichomfanya alale kwa muda na nguvu ya dawa ilipokwisha alishtuka na kumkuta daktari huyo akiendelea kumbaka.
“Baada ya kumkuta daktari akimbaka, mgonjwa huyo alitoka na kukimbilia Kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama na kufungua jalada lenye namba RB/KJN/123/552/10,” alieleza.
Alisema askari hao walirudi na mgonjwa huyo hospitali na kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa bado yupo eneo hilo.


0 comments