Vyanzo vya kiusalama vimesema, raia watatu wa Uingereza na mmoja kutoka Colombia wamekamwata katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta nchini Nigeria.
Watekaji nyara hao waliwakamata watu hao wanne karibu na bandari ya Harcourt, na kumwuua mlinzi ambaye ni raia wa Nigeria.
Eneo hilo la Niger Delta ni maarufu kwa utekaji nyara unaofanywa na wapiganaji, wanaotaka sehemu ya utajiri huo.
Lakini eneo hilo limekuwa na utulivu tangu makundi ya wapiganaji walipokubali kusalimisha silaha mwaka jana baada ya serikali kukubali kuwapa msamaha.
0 comments