Chelsea yatamba FA licha ya washambuliaji kusafiri | ||||
Mabingwa watetezi Chelsea wameanza vyema kampeni la kutetea kombe la FA baada ya kuishinda Watford mabao 5-0. Daniel Sturridge aliifungia Chelsea bao la kwanza katika dakika ya tano, la pili likawa la kujifunga na mengine yakafungwa na Florent Maluda na Frank Lampard. Safu ya ushambuliaji ya Chelsea ilitamba sana licha ya kuondokewa na Didier Drogba, Michael Essien, John Obi Mikel na Salomon Kalou ambao wamekwenda kuziwakilisha nchi zao katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika. Nicolas Anelka pia ana jeraha. |
You Are Here: Home - - Chelsea yatamba FA licha ya washambuliaji kusafiri
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
0 comments