KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amemtaka mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwataja kwa majina vigogo wa CCM wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.
Juzi, Profesa Lipumba alinukuliwa na vyombo vya habari(si Mwananchi) akisema anazo taarifa nyeti na za kweli kuhusu vigogo wa CCM wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.
“Hii ni nchi inayofuata sheria, hivyo kama Profesa Lipumba anao ushahidi na majina ya hao vigogo wa CCM wanaojihusisha na dawa za kulevya awataje,†alisema Makamba jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu huyo alisema endapo Profesa Lipumba atawaweka hadharani vigogo hao, atakuwa amelisaidia jeshi la polisi kutimiza wajibu wake.
“Ni muhimu Profesa Lipumba akawataja hao vigogo na atoe ushahidi ili polisi wafanye kazi yao,†alisema
Akizungumza juzi katika ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu la Taifa la CUF, Profesa Lipumba alisema anazo taarifa nyeti kutoka ndani ya CCM, kwamba vigogo wengi wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
0 comments