Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - BAADA YA WASOMI WA UNIVERSITY YA CHUO KIKUU CHA UDSM KUGOMA, MAMBO SI MAMBO, WATAKIWA KUJISAJILI UPYA. ASILIMIA KUBWA YATEMWA..

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), kimeongeza muda wa wanafunzi kutuma upya maombi ya udahili chuoni hapo, hadi Januari 29 mwaka huu.

Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho uamuzi huo unalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi kukamilisha uwasilishaji wa kiwango cha ada wanachostahili, kutoa kwa mwaka wa masomo 2008/09 kabla ya kuruhusiwa kujiunga na masomo katika muhula huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema" Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeongeza muda wa wanafunzi kutuma upya maombi ya udahili chuoni hapo, hadi Januari 29 mwaka huu."

Awali, wanafunzi hao walitakiwa wawe wametimiza masharti ya udahili wao tangu Januari 2 mwaka huu.

Akizungumzia kufunguliwa kwa vyuo hivyo Mukandala alisema majina ya wanafunzi waliotimiza masharti yote ya kudahiliwa upya tayari yameingizwa katika tovuti ya chuo hicho na kuwataka wanafunzi kuanza upya udahili kesho.

"Majina ya wanafunzi ambao tayari wametimiza masharti yote ya kudahiliwa upya yamewekwa kwenye tovuti ya chuo na kuanzia Jumatatu (kesho) wanafunzi wanatakiwa waanze udahili upya," alisema Profesa Mukandala.

Alibainisha kuwa kila mwanafunzi atatakiwa kuvaa kitambulisho chake kipya na kwamba hakuna mwanafunzi atakayeruhusiwa kuingia bwenini, darasani au kwenye mihadhara bila kuvaa kitambulisho hicho.

Alisema itakuwa ni uvunjaji wa sheria kwa mtu yeyote kuingia chuoni bila kitambulisho halali au ruhusa maalumu.

Katika hatua nyingine, Profesa Mukandala ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa za kufutwa kwa Chama cha Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO) na kueleza usahihi ni kwamba chama hicho hakijafutwa.

Alifafanua kuwa kimsingi kwa kanuni na taratibu za chuo hicho baada ya kusimamishwa masomo, wanafunzi wote walipoteza udahili wao.

Aliongeza kutokana na kutokuwepo wanafunzi halali wa chuo hicho, wote waliokuwa viongozi wa Daruso nao pia walipoteza nyadhifa zao za uongozi.

"Kwa mantiki hiyo, itakuwa kinyume cha sheria kwa mwanafunzi yeyote kufanya chochote kile kwa kisingizio cha kuwa kiongozi wa wanafunzi aliyechaguliwa," alisema Mukandala.

Wakati Mukandala akisisitiza hivyo aliyekuwa Rais wa Daruso, Anthony Machibya amepingana na kauli hiyo na kusema, wao bado ni viongozi halali na wenye mamlaka hivyo uongozi wa chuo hauwezi kuwafuta kwa kuwa hauna mamlaka hayo.

Alisema wao ni wanafunzi halali wa chuo hicho na kuwataka wanafunzi wote waliosimamishwa masomo kurudi chuoni, punde taarifa kufunguliwa chuo zikiwafikia kwani wao pia ni wanafunzi halali wa UDSM.

Kuhusu rufaa za wanafunzi ambazo Waziri wa Elemu na Mafunzo ya Ufundi, Jumanne Maghembe amedai zipelekwe kwake, Machibya alisema waziri huyo anadanganya kwa kuwa tayari anazo rufaa nyingi za wanafunzi mkononi mwake kwa muda mrefu na hajatoa majibu kwa rufaa hata moja.

Machibya pia alishangaa waziri huyo pamoja na Profesa Mukandala kueleza kuwa wanafunzi wengi wametimiza masharti bila kutoa idadi yao kitu ambacho kinaonyesha kutokufanyika vitu kwa umakini.

Alisema kwa takwimu ambazo serikali yake inazo ni kuwa kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanafunzi waliotimiza masharti ni 3,100 kati ya wanafunzi 11,300 kitu ambacho kinaonyesha wengi watabaki nyumbani.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Umma (Uvijuta), Silinde David, alisema wanafunzi waliofukuzwa vyuoni walikuwa ni 31,443 na hadi hivi sasa walioweza kulipa ni asilimia 13 ya wanafunzi hao huku asilimia 87 ambayo ni sawa na wanafunzi 27,289 hawajalipa.

Tags:

0 comments

Post a Comment