|
Bw Mbeki alikana kuingilia kesi ya Zuma |
Mwezi uliopita, hakimu Chris Nicolson alifuta mashitaka yaliyokuwa yakimkabili Bw Zuma.
Hakimu huyo alipendekeza kwamba mpinzani wake aliyekuwa rais wa nchi hiyo Thabo Mbeki aliingilia kesi hiyo.
Hukumu hiyo ilitoa fursa kwa chama tawala cha African National Congress, ANC kumwondosha Bw Mbeki madarakani.
Bw Zuma amekana mashitaka ya kuhusika na rushwa, ulanguzi wa fedha na ulaghai.
Wakati akitoa hukumu hiyo mwezi uliopita, Jaji Nicolson alisema waendesha mashitaka wangeshauriana na Bw Zuma kwanza kabla ya kumshitaki upya.
Waandishi wamesema hatua hizo za kisheria zinaweza kurudisha nyuma jitihada za Bw Zuma anayepewa nafasi kubwa ya kuwa rais wa nchi hiyo baada ya uchaguzi utakaofanyika mwakani kukwama.
0 comments