Wengine walioingia na umri mdogo ni mbunge mteule wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika ambaye ana umri wa miaka 29, Mwalimu Julius Nyerere ambaye alishinda uchaguzi wa Septemba 1957, Kabwe Zitto wa Chadema aliyekuwa kijana zaidi kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 kwenye Jimbo la Kigoma Kaskazini, Jakaya Mrisho Kikwete wa CCM kwenye Jimbo la Bagamoyo mwaka 1990, David Kafulila wa NCCR-Magezi ambaye alishinda kiti cha Kasulu Kaskazini mwaka 2010, Edward Vincent Nyerere wa Chadema kwenye Jimbo la Musoma Vijijini mwaka huu, Alfred Rulegura wa Tanu kwenye uchaguzi wa mwaka 1965 na Musobi Mageni wa Tanu kwenye Jimbo la Kwimba Kusini mwaka 1965.
Kwa kumuangalia kwa juu juu, unaweza kufikiri ni mpole na mkimya, lakini ni mtu anayetumia sauti yake nzito kujenga hoja thabiti na kuonyesha hali ya kujiamini sana na pengine ndicho kitu kilichomfanya aanze kupewa madaraka kwenye chama mapema. Aliingia NCCR-Mageuzi Februari 19, 2010. Aliitisha mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) wakati akiwa likizo fupi ya chuo na kutangaza rasmi kuwa amerudisha kadi ya Chadema na kuhamia NCCR. Siku hiyo aliitumia pia kukiponda chama chake cha Chadema na CCM, mbali na kutangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo hilo. Hilo liliwastua wengi kuwa atawezaje kufanya kazi kwa ushirikiano na wapinzani wenzake kama ana mtazamo tofauti kiasi hicho. "Misingi ya katiba ya nchi inampa mtu uhuru wa kuchagua chama au itikadi ninayoitaka ili mradi tu sivunji sheria au haki za wengine," alisema alipoongea na Mwananchi.
MWANAFUNZI ALIYESHINDA UBUNGE AKIWA NA UMRI MDOGO ZAIDI LAKINI ASILIMIA KUBWA YA KURA Na Denis Maringo KILA uchaguzi mkuu humalizika na mambo yake na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 umemalizika kwa Jimbo la Muhambwe kuwa na mshindi mwenye rekodi nyingi na za aina yake.
Kwa kawaida uchaguzi wa ubunge huambatana na matukio tofauti, ikiwa ni pamoja na kukataliwa kwa matokeo, mshindi kupingwa mahakamani na matokeo kubatilishwa na mahakama.
Lakini ushindi wa Felix Mkosamali kwenye Jimbo la Muhambwe haukuwa na matukio hayo ya kukataliwa au kufikishwa mahakamani, lakini wenye rekodi za aina yake baada ya kijana huyo mdogo kuibuka kuwa mshindi mwenye umri mdogo kuliko wote; aliyepata kura nyingi kuliko mshindi mwingine yeyote; mbunge wa kwanza kutoka upinzani kutwaa jimbo hilo; na mtu wa kwanza kushinda kiti cha ubunge akiwa anasoma nje ya jimbo lake na pia kushinda akiwa kwenye chama ambacho hakijawahi kuwa na mbunge.
Mkosamali, ambaye alizaliwa Juni 24, 1986 na ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa sheria anayeingia mwaka wa mwisho kwenye Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (Mwanza), alipata ushindi mkubwa kuliko wa mgombea yeyote aliyeshinda mwaka huu.


0 comments